Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Norway na klabu ya Manchester City Erling Braut Haaland ni rasmi sasa amerejea katika mazoezi baada ya kuwepo nje tangia mwezi disemba tarehe 6 alipopata jeraha kwenye mechi kati ya Manchester City na Aston Villa.
Hii ni dalili nzuri kwa mkufunzi Pep Guardiola ambaye analenga kuimarisha kikosi chake ili kutetea ubingwa msimu huu ikizingatiwa pia Kelvin De Bruyne amerejea katika kikosi rasmi baada ya kukaa mkekani kwa muda.
Kufikia sasa Haaland amefunga mabao 19 msimu huu na mchango wake unaonekana kuwa mkubwa Etihad. Kwa sasa Manchester City imesalia na alama 5 pekee kuwafikia vinara wa ligi Liverpool walio na alama 45 huku Manchester City pia ikiwa na mechi kiporo.

