ESSE AKIDA KUFANYA MASHINDANO YA SOKA KILA MWAKA KILIFI

Mchezaji wa timu ya taifa ya Harambe Starlets Essie Akida anasema kwamba mafanikio alopata kwenye soka si hapa nchini pekee bali hata kimataifa yanampa motisha wa kupenda kurudisha mkono kwajamii ilomkuza.

Akida ambaye kwa sasa anachezea klabu ya PAOK Thessaloniki katika taifa la ugiriki ameyasema hayo baada ya kuandaa mashindano ya soka mwezi December mwaka jana, mashindano aloyataja kama njia moja ya kurudisha shukrani pamoja na kukuza vipaji vya jamii mashindano aloyaandaa katika uwanja wa mkoroshoni.

”Nimeamua kuandaa mashindano haya ili kurudisha mkono kwa jamii ilonikuza. Mimi nimekulia hapahapa Mkoroshoni na nimecheza soka mashinani kama wengine kwa hivyo nafurahia kufanya mashindano kama haya.” Alisema Akida.

Mchezaji huyo wa zamani wa klabu ya Moving The Goal Post yenye makazi yake katika kaunti ya kilifi anasema anapania kufanya mashindano kama hayo kila mwaka huku akitoa wito kwa wanamichezo lakini pia wadhamini kujitokeza ili kusaidia kutimiza ndoto za vijana mashinani.

”Natoa wito kwa wadhamini wajotokeze wakati mwengine tufanye mambo kama haya zaidi lakini pia kuyaboresha.” Aliongeza Akida.