Wafanya biashara wa boraboda mjini Malindi wameomba waandalizi wa mashindano ya soka kuyafanya mara kwa mara kwani jambo hilo limechania pakubwa kuleta utangamano katika jamii.
Akizungumza na tama la spoti Hezron Mwaka ambaye ni kocha wa timu ya bodaboda ametoa wito huo baada ya mechi ya kirafiki ilochezwa wikendi ilopita dhidi ya kikosi cha maafisa wa polisi mechi ilotamatika 4-2.
”Tunatuma wito kwa waandaaji wa mashindano haya kuwa waendelee kuyafanya mara kwa mara. Jambo hili kwa kweli limetusaidia sana sisi kama bodaboda kwa sababu linaleta utangamano unaofaa.” Alisema Mwaka
Kwa upande wake Amani Ponda ambaye ni mchezaji wa kikosi ch polisi amewahimiza wachezaji kuzidisha mazoezi ili kujiimarisha kwa mashindano kama hayo siku za usoni.

