Waziri wa michezo hapa nchini Kenya Ababu Namwamba amesema kuwa anaimani mwaka huu utakuwa na ufanisi mkubwa katika michezo sawa na ilivyokuwa mwaka jana ambapo mashindano pamoja na wachezaji waliwakilisha na kushinda matuzo mbalimbali.
Amesema kwa kipindi cha mwaka jana pekee serikali iliwekeza milioni 900 katika michezo tofauti ya miaka ya nyuma ambapo michezo ilikuwa na mgao mchache wa kifedha.
Ametoa hakikisho kwa taifa kuwa mwaka huu serikali inalenga kuendeleza mawindo ya talanta mashinani huku ikiwa na malengo ya miaka ya baadaye kama vile kusuka kikosi cha Harambe Stars kwa ajili ya mashindano ya Afcon 2027.
Hata hivyo Ababu amesema kuwa ujio wa Talanta Hela kutasaidia zaidi kuimarisha michezo mashinani katika mawindo ya talanta. Vilevile kabla ya kutamatika mwaka jana serikali ilikuwa imetoa taarifa kuwa inalenga kutumia wachezaji wakongwe kama maskauti mashinani.

