Klabu ya Beach Bay inalilia udhamini wa kusimamia mechi zao kutokana na ukata wa kifedha unaowapa changamoto kubwa kwa sasa.
Klabu hiyo inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili ni kati ya vilabu vingi vinavyo kumbwa na changamoto hiyo kutoka mkoa huu wa pwani na Clara kadzo ambaye ni mweka hazina wa klabu hiyo anasema kwamba wachezaji wake wikendi ilopita walilazimika kucheza mechi mbili kuepuka garama za usafiri na chakula katika kaunti ya taita taveta.
”Kwa kweli tunapitia kipindi kigumu sana. Wikendi ilopita tulicheza mechi mbili mfululizo katika kaunti ya Taita Taveta ili tusiingie hasara ya kurudi tena huko. Wachezaji wangu nakwambia Paps hawakula chakula wakatosheka. Walikula tu chai na mandazi mbili na kabla ya mechi ya piliniliwanunulia maziwa tu basi. Kwa kweli suala la pesa latupeleka mbio. Tunahitaji udhamini na hivi karibuni tunataka kupanda mchango ili kusaidia hii hali.” Alisema Clara
Wikendi ilopita Beach Bay ilisajili alama nne ugenini alama moja kwenye sare dhidi ya Jr FC na tatu dhidi ya Kamtonga fc. Ikumbukwe kwamba kesho Beach Bay itakuwa inashuka dimbani dhidi ya klabu ya Mbungoni fc katika uwanja wao wa nyumbani huko mjanaheri, magarini kaunti ya kilifi.

