Klabu ya Mere fc licha ya kupoteza mechi yao jana katika uwanja wa nyumbani dhidi ya Arrow Head kwa kichapo cha mabao 3-2 inazidi kuongoza ligi ya eneo bunge la Malindi kaunti ya Kilifi kwa alama 35 alama moja mbele ya Real Galana walio katika nafasi ya pili na mechi moja mkononi.
Samuel Koi wa klabu ya Real Galana anazidi kumtoa jasho Bernanrd Thuva kutoka Kathama FC kwa mabao huku wote wakiongoza kwa mabao 10.
Kule Magarini ni kwamba Majenjeni Elites walilazimishwa sare tasa na wenyeji wao Super Eagles. Kwa sasa Majenjeni Elites wanasimama katika nafasi ya pili ligini wakiwa na alama 43 alama moja nyuma ya viongozi Green Mamba.
Bosuster kwa upande wa eneo la Gongoni wanazidi kuongoza ligi hiyo wakiwa na alama 50 baada ya kusajili ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya klabu ya Kikwathani katika uwanja wa Hope Fc.
Matokeo mengine ni kwamba
Amani fc vs Babylon 0-0
Hope fc vs White Stars 1-1
Venus vs Fundisa fc 1-3

