Bondia wa Kenya Daniel wanyonyi amemuonya mpinzani wake karim mandonga bondia kutoka Tanzania kwamba anamnyamazisha mdomo wake kabisa pindi wakikutana ulingoni katika pigano la marudinao jumamosi ijayo.
Mwezi machi mwaka huu katika pigano la kwanza Mandonga alipata ushindi dhidi ya Wanyonyi lakini safari hii mwenyeji amekataa katakata kupoteza mechi katika ardhi ya nyumbani.
Wanyonyi amesema amemtayarishia Mandonga ngumi ya kikenya kwa jina ‘Dusra’.
Karim Mandonga anatarajiwa kutua hapa nchini usiku wa leo kutoka Tanzania mwendo wa saa mbili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jkia.

