Harry Maguire ambaye amekuwa nahodha wa klabu ya Manchester United kule uingereza atapokonywa unahodha huo hata ikitokea hajauzwa msimu huu.
Majarida kadhaa yameripoti kwamba huenda Bruno Fernandes akapewa kitambaa hicho au Casemiro kuelekea msimu ujao.
Harry Maguire kwa sasa ameonekana hayupo kabisa katika mipango ya mkufunzi Erick Ten Hag na amewekwa mnadani huku vilabu kadhaa vya Uingereza ikiwemo Newcastle na Totenham Hotspurs zikiongoza katika kuwinda sahihi yake.
Wakati hayo yakijiri uhamisho wa kipa wa Cameroon Andre Onana wa pauni milioni 43 kutoka Inter Milan kwenda Manchester United uko katika hatua za mwisho na utakamilika wiki hii baada ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kukubaliana maslahi binafsi.
Manchester United pia wameweka thamani inayotakiwa ya £50m kwa klabu inayotaka kumnunua beki wa England Harry Maguire, 30.

