Mkufunzi wa klabu ya Beach Bay Peter Mole anasema kwamba amekuwa akitumiwa maombi mengi ya vilabu mashinani lakini pia mkoa wa pwani vikiomba huduma zake baada ya kujiuzulu mwezi juni kutoka wadhifa wake wa ukocha.
Kwa sasa mkufunzi huyo anajihusisha na kuiongoza timu ya shule ya upili ya Galana Boys huku akijipa likizo ya mashindano ya ligi za fkf anapowaza ni klabu gani atajiunga nayo.
Tetesi mashinani zasema kwamba ni mkufunzi anayelengwa sana na klabu ya Furunzi fc ambayo haina mkufunzi kwa sasa au ajiunge na klabu ya Inter Dabaso ambayo taarifa za soka la Kilifi zasema kwamba analenga kujiuzulu kutoka klabu hiyo.
Hata hivyo Peter Mole ameweka bayana matakwa yake kwa vilabu vinavyotaka huduma zake iwapo atakubali kusajiliwa na klabu yoyote.
Mkufunzi huyo alijiuzulu kutoka uongozi wa klabu ya Beach Bay kutokana na kukosa kuelewana katika uongozi pamoja na kuwa na migawanyiko miongoni mwa wachezzaji wa klabu hiyo ya Magarini kaunti ya Kilifi inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili.
Wakati hayo yakijiri baadhi ya wakufunzi mashinani wameanza kuonesha nia ya kujiuzulu na kuachana na soka kutokana na kukatishwa tamaa na kukosa usaidizi kimichezo katika serikali ya kaunti ya Kilifi.
Nero Chishenga amesema kwamba kunafununu kuwa wakufunzi wa soka wanapitia kipindi kigumu katika michezo licha ya kwamba hawafaidiki kiuchumi katika hali yoyote.
Amelilia gharama ya juu ya kuendesha ligi katika vilabu jambo ambalo linafanya baadhi ya timu kupitia changamoto zinazopelekea kukosa kuheshimu ratiba au vilabu kuvunjika na wachezaji kupotea mitaani kwenye mihadarati na kadhalika.

