HONG KONG YAWASILI KENYA KWA MASHINDANO YA MATAIFA MANANE

Timu ya raga ya chipukizi ya Hong Kong China ndiyo ya kwanza kuwasili nchini kwa mashindano ya timu nane yatakayoanza tarehe 15 jijini Nairobi.

Timu hiyo iliwasili jana usiku na itafungua mashindano hayo na mechi dhidi ya timu ya taifa ya Uhispania. Hong Kong China iko kundi moja na uhispania, Samoa na wenyeji Kenya.

Baada  ya mechi ya Hong Kong china dhidi ya uhispania tarehe 15 mwezi huu, itakabiliana na Samoa siku tano baadaye kisha ikamilishe mechi za makundi dhidi ya wenyeji Kenya tarehe 25 mwezi huu katika uwanja wa kimataifa wa Nyayo.

Timu hiyo ilianza kambi ya mazoezi wiki moja ilopita na imekusanya wachezaji kutoka nchi kumi duniani zikiwemo uingereza, new Zealand, Australia lakini pia Hong Kong.

Washindi wa michuano ya Nairobi mwezi huu watafuzu moja kwa moja katika daraja la kwanza la shirikisho la raga duniani World Rugby mwaka 2024.