Wito umetolewa kwa wazazi kuwahimiza watoto wao kuzingatia ukuzaji wa Talanta zao kama njia moja ya ufanisi wa maisha yao ya baadaye.
Akizungumza na Tama La spoti Bwana Mcdonald Mzungu ambaye ni katibu mkuu wa michezo ya shule za upili katika gatuzi la Kilifi ameshauri wazazi na walimu kuwahimiza wanao kuzingatia michezo ambayo pia ni ajira itakayotumika kuwatoa katika maisha ya uchochole.
Kwa sasa mashindano ya shule za upili yanendelea katika shule ya upili ya wavulana ya Marafa eneo bunge la Magarini na leo yamekuwa katika hatua ya mchujo lakini kesho ni robo fainali na hatimaye fainali kuchezwa jumamosi ambapo wawakilishi wa kaunti watakao ingia hatua ya kimkoa mashindano yatakayofanyika Voi Taita Taveta watabainika.

