Kiungo wa zamani wa timu ya taifa Haramber stars Douglas Mutua amesajiliwa rasmi kuwa mkufunzi mpya wa klabu ya Bandari fc yenye makazi yake Mbaraki Sports club Mombasa.
Mutua sasa atakuwa anachukua mikoba ya uongozi wa klabu hiyo ya Mombasa kutoka kwa Muhiddin aliyekuwa anashikilia kwa muda.
Wakati uo huo mkufunzi wa zamani wa Sofapaka John Baraza atakuwa anaungana na Mutua katika klabu ya Bandari kama naibu mkufunzi wake.
Msimu uliopita klabu ya Bandari ilimfuta kazi mkufunzi wake Anthony Modo Kimani kutokana na matokeo mabaya na kumpa kazi Muhhiddin kuiongoza klabu hiyo hadi mwisho wa msimu.
Bandari ilimaliza msimu iliopita katika nafasi ya katika nafasi ya sita na alama 34. Hassan Abdallah ndiye aliyemaliza kama mfungaji bora wa klabu hiyo akiwa na mabao 13.

