PETER MOLE YUPO SOKONI BAADA YA KUACHANA NA BEACH BAY

Mkufunzi wa klabu ya Beach bay Peter Mole amethibitisha kwamba ameachana rasmi na klabu hiyo inayoshiriki katika ligi ya daraja la pili kitaifa kutokana na kutoelewana baina ya uongozi wa klabu hiyo pamoja na mgawanyiko ulioko miongoni mwa wachezaji.

Amesema kwamba kwa sasa yupo huru kuungana na klabu mpya na wiki hii amehusishwa katika kuiongoza timu ya shule ya upili ya Galana katika mashindano ya shule za upili hatua ya kaunti ya Kilifi yanayoendelea katika shule ya upili ya wavulana ya Marafa.

Kati ya sababu zilizomfanya Peter Mole kuachana na Beach Bay ni wachezaji kuzembea katika mazoezi jambo ambalo lilikuwa halimpi motisha.

Naam hii leo timu Galana Boys inayoongozwa na mkufunzi huyo imetolewa katika hatua ya robo fainali dhidi na shule ya Upili ya wavulana ya MALINDI High.