Shirikisho la soka nchini Kenya limetangaza kwamba kuelekea msimu ujao makocha wote wanaoongoza timu za ligi kuu ya fkf watafaa kuwa na vyeti vya ukocha katika kiwango cha Caf B.
Nick Mwendwa ambaye ni rais wa shirikisho la fkf ameyasema hayo kipindi ambacho sasa kuna mafunzo ya ukocha yanaendelea kote nchini ili kuona kwamba soka linaimarika hata zaidi.
Kulingana na Mwendwa ni kuwa misimu iliyopita FKF imekuwa ikiruhusu makocha wenye viwango vya CAF C kuongoza vilabu vya ligi kuu ya fkf premier league lakini sasa msimu wa mwaka 2023/2024 utakuwa na lazima makocha wawe na CAF B.
Mafunzo ya ukocha wa CAF B yalianza rasmi jumatatu wiki hii jijini Nairobi na rais Mwendwa ametoa wito kwa walimu wa shule za upili pamoja na zile za msingi kujihusisha na mafunzo ya ukocha ili kusaidia makuzi ya talanta za wachezaji katika umri mchanga.
Hata hivyo ameeleza kufurahishwa kwake na kuona baadhi ya walimu wakiwa miongoni mwa wanafunzi wa CAF B wiki hii.

