TIMU ZA ENEO BUNGE LA MALINDI KUINGIA KAUNTI ZIMEBAINIKA

Shule ya upili ya wavulana ya Malindi pamoja na ile ya kinadada ya Kakoneni ndio shule zilizofuzu kutoka mashindano ya mpira wa soka eneo bunge la Malindi kaunti ya kilifi na sasa kuingia katika mashindano ya hatua ya Kaunti.

Katika mchezo wa Voliboli shule ya upili ya Mekatilili pamoja na shule ya Barani zilifuzu kuwakilisha eneo bunge la Malindi. Mchezo wa Netiboli Malindi itawakilishwa na shule ya Upili ya kibokoni na hatimaye raga ikiwakilishwa na shule ya upili ya Malindi.

Akizungumza na Tama la Spoti  Samuel Mulati ambaye ni katibu mkuu wa michezo ya zule za upili eneo bunge la Malindi amesema kwamba kwa sasa katika kaunti ya kilifi, mchezo wa raga umeanza kuongezeka washiriki tofauti na miaka ya nyuma.

Mashindano hayo yatarejea mwezi julai katika hatua ya kaunti na kambi kuu sasa itakuwa shule ya upili ya Marafa iliyoko eneo bunge la Magarini.