GOR MAHIA YAZIDI KUZAWADIWA BAADA YA KUBEBA UBINGWA

Waziri wa mawasiliano Eliud Owalo amewazawidi Kogalo shilingi milioni 3 ambao wameshinda ubingwa wao wa 20 katika ligi kuu ya fkf hapa nchini Kenya.

Hii ni baada ya Gor Mahia kuitandika Nairobi City stars kichapo cha mabao 4-1 katika uwanja wa moi kasarani na kushinda ubingwa huo.

Owalo pia amewaahidi Kogalo basi jipya wanapoelekea msimu ujao kutokana na kuwa na kiwango bora msimu huu kwenye ligi ya fkf.

Awali Gor Mahia walikuwa wamezawadiwa shilingi milioni 3.5 na kampuni ya ubashiri ya sportpesa kwa kushinda ubingwa huo.

Haya yanajiri kipindi ambacho kumekosa kuonekana juhudi za kuwatuza mabingwa kutoka kwa fkf ambao wanakiongozwa na Nick Mwendwa walisema kwamba hakuna hela za kutuza mabingwa msimu huu kutokana na kukosa mdhamini wa ligi.