Klabu ya Barcelona ambao ni mabingwa wa Laliga kule uhispania wamekubaliana na Ikkay Gundogan ambaye ni nahodha wa klabu ya manchester city walioshinda kombe la mabingwa ulaya pamoja na ligi kuu nchini Uingereza.
Gundogan alikuwa amepewa ofa ya kuongeza uwepo wake katika dimba la Etihad lakini ameamua kuihama kambi hiyo na kujiunga na kambi ya Xavi Herdandez.
Gundogan mwenye umri wa miaka 32 alisajiliwa na Manchester City kutoka Borrussia Dortmund mwaka 2016 na akiwa na Pep Guardioala amecheza mechi 300 katika ligi zote.
Kim Min-Jae, mchezaji anayelengwa sana na klabu ya Manchester United na klabu ya Bayern Munich ataendeleza mchakato wa uhamisho baada ya kupokea mafunzo ya kijeshi katika taifa lake la Korea Kusini.
Ikumbukwe kwamba ni sharti katika taifa hilo kwa kijana wa kiume kuingia kwenye mafunzo ya kijesi kwa kipindi cha kati ya miezi 18 hadi 21 anapofikisha umri wa miaka 18 hadi 28.
Kufikia sasa Bayern Munich ndio klabu inayoongoza katika mbio za kumsajili Kim kutoka Napoli.

