WADAU WA ELIMU WAHIMIZA MAKUZI YA TALANTA CHANGA

Naibu katibu mkuu wa Kuppet katika kaunti ya Kilifi  bwana Oppolo K’opollo amewahimiza wazazi kusaidia wanao kukuza talanta katika umri mchanga.

Oppolo amesema kwamba katika cha michezo ya shule za msingi lakini pia za upili ndio kipindi ambacho talanta za vijana hugunduliwa na kuna urahisi wa mchezaji kuanza kujenga kipaji chake.

Katibu huyo amewashauri wazazi wenye wanafunzi wao mashuleni wanafaa kuwaruhusu kurindima michezo mbalimbali pamoja na talanta ambazo huenda zikawafaa katika maisha ya baadaye.

”Kuna umuhimu kwa wazazi kuhimiza wanawao kuzingatia michezo, kusaidia kukuza talanta zao wakiwa wachanga. Umri wa miaka hii wakiwa shule za upili na hata msingi hapo ndipo kwenye urahisi kwa talanta kugundulika.” Alisema Oppolo

Kulingana na Kopollo ni kwamba michezo si jambo la kubezwa kwani lina uwezo wa kubadilisha maisha ya vijana wengi pamoja na jamii kwa jumla.

Ametolea mfano wachezaji kama Michael Olunga, Collins Injera lakini pia wanariadha wa Kenya ambao wanapiga mpunga mrefu kupitia michezo.

”Ukiangalia watu kama vile Michael Olunga, Collins Injera na hata wanariadha wa Athletics Kenya walianza wakiwa na umri mchana. Saa hii ukiwatazama wanaishi vizuri na yote hiyo ni kupitia michezo. Kwa sababu walianza kitambo kufunzwa michezo.” Aliongeza Oppolo