NKUNKU ASAJILIWA NA CHELSEA, MANCHESTER UNITED NA PSG ZIKIMWINDA HARRY KANE

Klabu ya Chelsea hii leo imethibitisha kuwa Christopher Nkunku atakuwa mchezaji wao pale darajani Stanford Brigde baada ya kukamilisha usajili wake kutoka klabu ya RB Leipzig ya Ujerumani.

Nkunku ametia saini mkataba wa miaka sita baada ya makubaliano ya uhamisho wa pauni milioni 52.

Nkunku ameifungia mabao 16 waajiri wake wa zamani RB Leipzig pamoja na assists sita katika mechi 25 za ligi ya Bundesliga.

Paris St-Germain wamemfanya mshambuliaji wa Tottenham na Uingereza Harry Kane, 29, kuwa kipaumbele chao msimu huu baada ya kuondoka kwa mshambuliaji wa Argentina Lionel Messi, 35.

Pia Harry Kane amekuwa akiwindwa sana na klabu ya Manchester United ambao kwa sasa wanaangalia uwezekano wa kumnasa muingereza huyo iwapo jaribio lao la kumpataVictor  Osemhen kutoka klabu ya Napoli litafeli.