LAMU YAPIPANGA KWA TALANTA HELA

Mashindano ya Talanta Hela yatakayo dhaminiwa na Rais William Samoei Ruto yanayohusisha wachezaji wa soka wasiozidi umri wa miaka 19 kutoka kaunti zote 47 yanazidi kuvutia vilabu vingi mashinani.

Kaunti ya Lamu wikendi hii iliandaa mashindano ya kutafuta wachezaji  kutoka wadi zote za kaunti hiyo watakao shiriki katika mashindano hayo ya mwezi disemba tarehe 12 siku ya Jamhuri jijini Nairobi.

Kulingana na gavana wa kaunti ya Lamu Issa Timamy ni kwamba matayarisho kabambe ya kuchagua kikosi yanazidi kunoga na wamehusisha wakufunzi ambao wanasaidia katika kikosi hicho ambacho huenda wakakitaja katika siku chache zijazo.

Sebastian Owanga ambaye ni waziri wa Elimu katika kaunti hiyo amesema kwamba kama kaunti wanajitahidi kuandaa timu thabiti ambayo italeta ushindani katika mashindano hayo makubwa mwishoni mwa mwaka huu akiwa na imani kwamba timu ya Lamu itamaliza katika fainali.