Klabu ya Deep Sea ambayo inaongozwa na mkufunzi Athman Pirezi kutoka kaunti Lamu wikendi hii imezawadiwa alama tatu baada ya klabu ya Shimanzi FC kukosa kuheshimu ratiba.
Kulingana na chapisho katika ukurasa wa Facebook ya Shimanzi FC ni kwamba klabu hiyo ilikuwa imetuma ombi kwa shirikisho mechi hiyo iarirshwe lakini ombi lao likakataliwa.
Shimanzi walishindwa kusafiri kutokana na ukata wa kifedha jambo ambalo limekuwa likikumba vilabu vingi mashianai hasa katika ligi ya daraja la pili kitaifa.
Wakati hayo yakijiri klabu ya Ashton Rangers wikendi hii walisajili ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Mariakani fc.
Kamtonga waliwalazimisha OmAX fc sare ya mabao 2-2 huku Sparki Youth wakiitandika Ziwani Youth kichapo cha mabao 2-0.
Katika uwanja wa Alaskan Furunzi fc walitandikwa kichapo cha mabao 2-0 dhidi ya Samburu na hatimaye Beach Bay ya mkufunzi Peter Mole ikitandikwa kichapo cha mabao 5-0 dhidi ya Simba Apparel.

