VIHIGA QUEENS NDIO MABINGWA WA FKFWPL

Klabu ya kinadada ya Vihiga Queens wametangazwa kama mabingwa wa ligi kuu ya fkf ya kinadada nchini baada ya kuwa na kiwango kizuri msimu huu.

Malkia hao wamesalia na mechi moja kutamatisha msimu wao mechi ambayo inafaa kurindimwa Jumamosi wikendi hii dhidi ya klabu ya Gaspo Women. Kwa sasa Vihiga wako na alama 52 alama nne mbele ya Gaspo Women.

Wakati hayo yakijiri uongozi wa klabu ya Gaspo umeandikia shirikisho la soka kwamba hawatashiriki katika mechi yao ya mwisho msimu huu dhidi ya Vihiga Queens kutokana na sababu zao binafsi.

Msimu huu 2022/2023 utakuwa unatamatika rasmi wikendi ijayo.