KISHADA YAVUNA ALAMA, FURUNZI IKIUGUA

Klabu ya Kishada FC katika ligi ya daraja la pili kitaifa imepewa alama tatu baada ya klabu ya Furunzi fc inayoongozwa na mkufunzi Nero Chishenga Kushindwa kulipa hela za kusimamia refa wa mechi yao jana katika uwanja wa shule ya Upili ya Joho Girls katika kaunti ya Mombasa.

Mechi hiyo ililazimika kusitishwa kabla kipindi cha pili kuanza rasmi kutokana na Furunzi FC kukosa kuwasilisha hela hizo kwa wakati unaofaa hiyo alama zote tatu kupewa Kishada FC ambao tayari walikuwa bao 1-0 mbele katika kipindi cha kwanza.

Vilabu vingi vya Kilifi vikitafunwa na makali ya ukata wa kifedha jambo ambalo limefanya vilabu hivyo kukosa kuandikisha matokeo mazuri katika siku za hivi punde.

Wakati hayo yakijiri klabu ya Beach Bay kutoka Magarini kaunti ya Kilifi inalenga kufanya mchango wikendi hii ili kuchanga hela za kuipiga jeki klabu hiyo wanapoelekea kuvaana na Simba Apparel siku ya Jumapili.