WACHEZAJI WALIA NJAA FURUNZI

Mkufunzi wa klabu ya Furunzi FC Nero Chishenga amesema kwamba ukata wa kifedha unazidi kudidimiza klabu yake jambo ambalo linawafanya kukosa kuandikisha matokeo mazuri katika ligi msimu huo ambao ndio wao wa kwanza katika ligi ya daraja la pili kitaifa.

Ameambia Tama la spoti kwamba wachezaji wake wanasafiri kucheza mechi za mbali wakiwa njaa, mbali na usafiri kuzidi kuwapiga chenga. Kwa sasa anasema wameanza mchakato wa kutafuta mbinu za  kudhamini klabu hiyo ili kumaliza msimu vizuri.

Mkufunzi huyo anasema kwamba wachezaji wake kwa sasa wameanza kuvunjika moyo kuendelea na michezo licha ya kuwahimiza kusalia uwanjani wanapozidi kupigana na changamoto walizonazo kwa sasa.