Mechi moja kubwa ya ligi kuu nchini uingereza itakuwa inarindimwa usiku wa leo. Manchester United ambao tayari wameshajihakikishia nafasi yao katika mashindano ya Uefa msimu ujao watakuwa wanawakaribisha Cheslea katika uwanja wa Old Trafford.
Manchester United katika mechi hiyo watakuwa wanamkosa Marcel Sabister, Van De Bleek pamoja na Lisandro Martinez wote wakiwa wanaugulia majeraha.
Upande wa Chelsea majeraha ndio mengi kwani pia watakuwa wanamkosa Ben Chilwell, Ngollo Kante, Mason Mount, Reece James, Marc Cucurela.
Mechi hiyo itachezwa mwendo wa saa nne usiku.

