FIRAT AKANA MADAI YA UPENDELEO

Mkufunzi mkuu wa timu ya taifa ya soka Harambe Stars Engin Firat amekanusha madai kwamba yeye amekuwa na upendeleo katika kuchagua wachezaji wa kuwakilisha taifa hili katika kikosi chake.

Firat amesema kwamba uteuzi wake unafanyika kulingana na viwango vya wachezaji watakaomfurahisha tofauti na madai ya baadhi ya mashabiki wa Kenya wanaosema anaangalia wachezaji wa vilabu vinavyoshiriki katika ligi kubwa za nje ya taifa hili.

Mkufunzi huyo raia wa Uturuki amesema kwamba analenga kuchagua vikosi kutoka kwa ngazi zote za soka hadi mashinani, almaradi mchezaji amemfurahisha katika mchezo.