HAALAND ASHINDA TUZO LAKE LA KWANZA UINGEREZA

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester City mwite Erling Braut Haaland ameshinda tuzo lake la kwanza tangu ahamie ligi kuu nchini uingereza akitokea klabu ya Borussia Dortmund.

Haaland ameshinda tuzo la mchezaji bora wa mwaka wa chama cha waandishi wa soka wa Uingereza.

Pamoja na hayo Haaland ameshinda tuzo la mchezaji bora wa mwezi April. Kufikia sasa Haaland amefunga mabao 35 ya ligi kuu nchini Uingereza pamoja na kutoa asisti saba wakati akiwa ameingia kambani mara 12 katika mitanangwe ya ligi ya klabu bingwa Ulaya.

Mkufunzi wa Aston Villa Unai Emery ameshinda tuzo la mkufunzi bora wa mwezi Aprili.