HII NDIO NAFASI NZURI YA KUJIUZA KAMA MCHEZAJI – BENSON OMALA

Klabu ya GOR Mahia ambao ndio viongozi wa ligi kuu ya Fkf  nchini watakuwa wanavaana na AFC Leopards wikendi hii katika daby ya mashemeji hao wawili itakayopeperushwa moja kwa moja na televisheni ya kitanzania Azam TV kama makubaliano na shirikisho la soka hapa nchini.

Benson Omala ambaye ni mshambuliaji anayetegemewa sana na klabu yake ya GOR Mahia amesema kwamba klabu yake iko Imara na tayari kwa mchuano huo mkubwa wikendi hii.

Omala ameongeza kwamba mechi hiyo ni kubwa kwa wachezaji wa Kenya hivyo ni nafasi nzuri ya kujiuza kwa soka la kimataifa.

“Game ya wikendi hii na AFC Leopards ni game kubwa kwa Kenya na ni game ambayo wakenya wengi wanaitazama. Kama player hii ni time poa ya kujiuza. Binafsi nalenga kuzidisha idadi yangu ya mabao wikendi hii pamoja na mechi ambazo zimesalia.” Alisema Omala