KILIFI KUWA WENYEJI WA MAKALA YA TISA YA KYISA MWAKANI

Waziri wa michezo na vijana katika kaunti ya Kilifi mwite Ruth Dama Masha anasema amefurahishwa sana na uamuzi wa wizara ya michezo kitaifa inayoongozwa na waziri Ababu Namwamba kuipa kaunti ya kilifi nafasi ya kuandaa mashindano ya Kenya Youth Inter County Sports makala ya tisa mwakani.

Hii ilitokana na ombi la kaunti ya kilifi kuandaa mashindano hayo ikizingatiwa kwamba kwa sasa ndio kaunti ya pekee kutoka mkoa wa pwani inayoshiriki makala ya nane ya KYISA yanayofanyika katika kaunti ya Tharaka Nithi, mashindano ambayo yameanza rasmi asubuhi ya leo.

Waziri Ruth amesema kwamba kama serikali ya kaunti kwa sasa wanalenga kuanza mchankato mzima wa kuanza kujenga viwanja vya hadhi ili kuwa wenyeji wa mashindano yako ya kitaifa ambayo kufanyika kila mwaka baada ya ombi lao kukubaliwa.