KAUNTI YA KILIFI YAZIDI KUJIANDAA KWA MASHINDANO YA KYISA THARAKA NITHI

Timu ya soka itakayowakilisha kaunti ya Kilifi katika mashindano ya kitaifa ya Kenya Youth Inter County sports yatakayofanyika katika kaunti ya tharaka Nithi yatakayoanza rasmi wikendi hii tarehe 23 hadi 30 mwezi huu wa Aprili inaendelea na maandalizi ya lala salama kujitayarisha kwa michuano hiyo.
Jana katika uwanja wa mpira wa MTG ulioko eneo la Mnarani kaunti ya Kilifi walishiriki katika mechi ya kirafiki dhidi ya Blue Blue fc na kupiga sare ya bao 1-1.
Timu hiyo yenye mchanganyiko wa talanta za kutoka maeneo bunge yote ya Kilifi, wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 imesema kwamba iko tayari kuwakilisha kaunti ya Kilifi kwa mashindano hayo na waziri wa jinsia, utamaduni na michezo kaunti hii mwite Ruth Dama Masha amekuwa mdau mkubwa ambaye amekuwa akiwatembelea kambini mwao kuwatia motisha wa kuonyesha vipaji vyao kwa manufaa ya kaunti na maeneo bunge yao.