LIGI YA KAUNTI YA MOMBASA KUREJEA BAADA YA MFUNGO

Ligi ya shirikisho ya kaunti ya Mombasa inatarajiwa kurejea wiki ijayo baada ya kusimama kwa muda kupisha mwezi wa mfungo wa Ramadhan.

Kulingana na shirikisho la soka la kaunti ya Mombasa ni kwamba mechi ya kwanza itakuwa ni ile ya klabu ya Goodhope dhidi ya Ushindi katika uwanja wa Khadija, mechi itakayochezwa tarehe 29.

Kabla ya kusimama kwa ligi hiyo Mvita walikuwa wanaongoza ligi wakiwa sare na Coast Stars kwa alama 12 baada ya mechi nne.