LIGI YA FKF KUANZA RASMI WIKENDI IJAYO – DICKSON ANGORE

Ligi ya kaunti ya Kilifi itaanza rasmi wikendi ijayo baada ya matayarisho ya muda mrefu na shirikisho la soka FKF.

Mwenyekiti wa shirikisho la fkf kaunti ya Kilifi Dickson Angore amesema kwamba matayarisho yamechelewa kutokana na usajili wa wachezaji katika orodha maalumu ya wachezaji katika Fifa Connect

Usajili huo umekuwa ukifanyiwa kwa upole na umakini ili kuondoa hali ya baadhi ya wachezaji kusajliwa na kuchezea vilabu zaidi ya moja.

Wakati hayo yakijiri baadhi ya vilabu vinavyo shiriki ligi za mashinani vimekuwa vikilalamika kuhusu suala la udanganyifu na maonevu kwani kuna wachezaji ambao wamekua wakishuhudiwa kuchezea vilabu zaidi ya moja.