Klabu ya Liverpool usiku wa kuamkia leo imesajili ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya LEEDS United katika uwanja wa Elland road kwenye ligi kuu ya primia Uingereza.
Liverpool inayoongozwa na mkufunzi Jergen Klopp ilipata mabao yake kupitia Cody Gakpo aliyefunga bao moja, Mo Salah bao mbili, Diogo Jota bao mbili na Darwin Nunez akiingia kambani katika dakika ya 90.
Huu unakuwa ushindi wa kwanza kwa Liverpool tangia iicharaze Manchester United bao 7-0 katika uwanja wa Anfield.
Kwa sasa Liverpool inasalia katika nafasi ya nane na alama 47, alama 9 nyuma ya “Top four” huku wakiwa wamesalia na mechi 8 kujitafutia nafasi ya kushiriki mitanangwe ya klabu bingwa UCL msimu ujao.

