Klabu ya Beach Bay katika ligi ya daraja la pili kitaifa wikendi hii ilipewa alama tatu na mabao 2-0 kutokana na klabu ya Sparki Youth kukosa kuheshimu ratiba.
Sparki Youth ilishindwa kusafiri hadi mjanaheri kutokana na ukosefu wa usafiri ikiwa ni mechi ya pili sasa mfululizo inakosa mechi baada ya kukosa kusafiri hadi taita taveta kuvaana na Kamtonga majuma mawili yalopita.
Katika dimba lengineni kwamba Yanga walipiga sare tasa dhidi ya Kishada, Furunzi ikikabwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Inter Dabaso ya watamu katika dabi ya kaunti ya kilifi ilochezwa katika uwanja wa Alaskan hapo jana na hatimaye Deep Sea ikitandikwa na klabu ya Kamtonga kichapo cha mabao 3-2.

