Ligi ya kaunti ya Kilifi licha ya kuchelewa kwake itaanza rasmi tarehe 22 mwezi april mwaka huu baada ya matayarisho ya muda mrefu yalochochezwa na uhaba wa hela kwa vilabu husika ambavyo vimechelewa kulipa ada ya kushiriki ligi hiyo.
Kulingana na Japhet Kaingu ambayeni katibu mkuu wa soka la kaunti ya kilifi anasema kwamba takriban vilabu 60 kutoka kaunti ya kilifi vitashiriki katika ligi hiyo.
Katibu huyo akizungumza na Tama La Spoti kupitia njia ya simu mchana wa leo amesema kwamba wikendi ijayo wanalenga kuchapisha rasmi ratiba ya ligi na hatimaye kusubiri siku ya kuongoa nanga.
Kwa upande wa vilabu vinavyosubiri kuanza kwa ligi hiyo wanalalamikia ahadi vyingi kutoka kwa uongozi wa fkf. Jasper Kazungu ambaye ni nahodha wa klabu ya Lubumbashy ambao ni mabingwa wa ligi ya eneo bunge la Magarini msimu jana anasema kwamba kwa sasa wanapiga mechi za kirafiki ili kujiweka imara wakisubiri ligi hiyo kuanza rasmi.

