Mashindano ya kombe la dunia yatakuwa yanarejea rasmi usiku wa leo katika hatua ya robo fainali na mechi mbili zimeratibiwa kurindimwa.
Benfica ya ureno watakuwa wanaikaribisha inter Milan ya italia katika dimba lao la nyumbani la Estado da Luz
Katika dimba la etihad Manchester City watakuwa wanawakaribisha miamba wa ujerumani Bayern Munich inayoongozwa na mkufunzi wao mpya Thomas Tuchel.
Mkufunzi mkuu wa Manchester City Pep Guardiola amesema kwamba msimu huu ana hamu kubwa ya kunyakua ubingwa wa kombe hilo.
Mkufunzi huyo Amekuwa na mafanikio makubwa katika klabu ya Manchester City lakini kombe ambalo amelisaza kuchukua ni Uefa baada ya kuwepo Uingereza kwa takriban misimu mitano sasa.

