TUTASAJILI WACHEZAJI WENYE TAJRIBA PEKEE – MWABATI

Mkurugenzi mkuu wa klabu ya Young Bulls Johnson Mwabati anasema kwamba amefurahishwa na hatua ambayo klabu yake imepiga msimu huu.

Kwa sasa klabu hiyo inaongoza ligi na alama 39 kwenye daraja la kwanza kitaifa na Mwabati anasema kwamba bado vijana wake wana njaa ya kusajili ushindi zaidi.

Wikendi ijayo Young Bulls watakuwa wanashuka dimbani dhidi ya klabu ya Dandora Youth jijini Nairobi.

Hata hivyo kiongozi huyo amesema kwamba changamoto ya kifedha bado inawaandama wanapojitayarisha kwa safari hiyo wikendi hii.