UHAMISHO WA DARAJA LA PILI KITAIFA

Mohamed Kazungu wa klabu ya Omax FC kutoka Mombasa, klabu inayoshiriki ligi ya daraja la pili kitaifa sasa ameajiliwa rasmi na klabu ya ligi kuu ya fkf Posta Rangers.

Ni mchezaji ambaye amekuwepo Omax kwa kipindi cha miezi minne pekee chini ya kocha Juma Kalato na alitambuliwa na Posta Rangers kupitia mechi ya Omax dhidi ya Mariakani fc.

Usimamizi wa Omax umethibitisha kuondoka kwa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 ambaye amekuwepo Posta Rangers kwa majiribio ya muda.

Wakati hayo yakijiri Omax inafuatilia saini ya John Fundi kutoka Kibera Soccer ili kuongeza kasi yao kwenye mashambulizi. Omax ni klabu inayoongoza ligi ya fkf katika daraja la pili kitaifa.