FKF WAMETUMIA BUSARA KUTUPIMA NGUVU NA IRAN, ASEMA OLUNGA

Timu ya taifa ya Harambe Stars iliwasili jana katika taifa la Iran kwa mchuano wa kirafiki dhidi ya timu hiyo inayosimama katika nafasi ya 24 ulimwenguni kote kwa mujibu wa viwango vya fifa kutokana kwamba pia mwaka jana ilishiriki katika mashindano ya kombe la dunia.

Kenya inayosimama katika nafasi ya 101 katika viwango vya fifa sasa itakuwa inacheza mechi yake ya kwanza ya kimataifa katika muda wa zaidi ya mwaka mmoja baada ya kufungiwa na fifa kutokana na serikali ilopita kuingilia masuala ya shirikisho la fkf.

Kwa mujibu wa Michael Olunga ambaye sasa ni nahodha wa kikosi hicho ameshukuru shirikisho la fkf kwa kuandaa mechi ya kirafiki baina ya taifa la Iran kwa kile anachokitaja kwamba ni mpinzani mzuri wa kushindana naye katika suala zima la kujipima uwezo wao kimataifa.