WAZAZI ENEO LA WATAMU WAHIMIZWA KUTHAMINI MASOMO YA WATOTO WAO

Wazazi katika wadi ya Watamu eneo bunge la Kilifi Kaskazini kaunti ya Kilifi, wametakiwa kuchukulia kwa uzito zaidi suala la masomo ya watoto wao ili kuhakikisha wananufaika maishani.
Wito huo umetolewa na baadhi ya viongozi katika wadi hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wa kamati ya fedha za WARD SCHOLASHIP FUND, Shebwana Mohammed pamoja na aliyekuwa mwakilishi wa wadi mteule katika serikali ya kaunti ya KIlifi, Barke Ali Mohammed ambao wametaja suala hilo kuwa changamoto kuu katika jamii eneo hilo.
Wakizungumza na lulu fm wamesema kuwa wazazi wengi hawajakuwa wakizingatia masomo ya watoto wao na kusisitiza kuwa wazazi katika dini ya kiislamu wanapaswa kuhakikisha wanawashauri watoto kusoma kwa bidii.