HASSAN OLE NADO AMTAKA RAIS RUTO KUTOJIBIZANA NA RAILA ODINGA

Katibu mkuu wa baraza kuu la waislamu nchini SUPKEM Hassan Ole Nado sasa ameitaka serikali kuu kuangazia changamoto zinazowakabili Wakenya na namna ya kuzitatua.
Kulingana na Ole Nado, gharama ya maisha inaendelea kuathiri maisha ya wengi na ni lazima mikakati iwekwe ili kuwanusuru Wananchi kwa sasa.
Amemtaka Rais William Samoei Ruto kutojiingiza katika majibizano baina yake na upinzani na badala yake kuendeleza mikakati ya kuliboresha taifa la Kenya.
Amesema majibizano yatachangia kwa taifa la Kenya kukosa kuafikia malengo yake ya maendeleo.