UHABA WA MAJI WADI YA GONGONI ENEO BUNGE LA GONGONI HUENDA UKAPATA SULUHU

Huenda wakaazi wa wadi ya Gongoni eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi wakapata suluhu la kudumu kutokana na uhaba wa maji kupitia afisi ya mwakilishi wa wadi hiyo Stephen Baya.
Kulingana na kiongozi huyo, wadi hiyo imekuwa ikikabiliwa na uhaba wa maji na kuwepo kwa barabara mbovu jambo ambalo, amesema ni sharti litatuliwe katika uongozi wake.
Aidha, ametaja vijiji vya Sosoni na Shomela kuwa mojawapo ya maeneo ambayo yamekuwa yakiathirika zaidi na ukosefu wa maji na hata barabara mbaya.
Kwa upande wake waziri wa maji kaunti ya Kilifi, Omar Said ameelezea kuwa serikali ya kaunti inapania kuanzisha mpango wa kusambaza maji kwa kutumia miale ya jua.