Mkufunzi wa timu ya taifa ya mpira wa wavu ya Malkia Straikas Paul Bitok ameeleza kuridhika na hatua ya kamati ya olimpiki nchini Noc kuandaa mashindano ya michezo ya ufukweni mjini malindi kaunti ya Kilifi wikendi ilopita.
Amesema hatua hiyo itasaidia kujenga vikosi vya kitaifa vitakavyowakilisha taifa hili kimataifa.
Mkufunzi huyo amesema anamatumaini makubwa kwamba taifa la Kenya litafuzu katika mashindano ya dunia baada ya mashindano yatakayofanyika nchini Tunisia mwezi juzi kuwinda tikiti hiyo.

