MANDONGA YWAREJEA KENYA NA ‘MLUNGAMBUNGA’ KAMA NGUMI YAKE MPYA

Mlungambunga ndio ngumi mpya atakayokuja nayo nchini Kenya Bondia wa Tanzania Karim Mandonga atakapokuwa anashuka ulingoni dhidi ya Kenneth Lukyamuzi raia wa Uganda.

Bondia huyo mwenye umri wa miaka 43 atapigana katika pambano la raundi kumi na mpinzani wake wikendi ijayo baada ya pambano la marudiano na Daniel Wanyonyi matayarisho yake kutibuka katika matayarisho.

Mandonga ameahidi mashabiki wake kwamba atasajili ushindi katika pambano la wikendi ijayo nchini Kenya, pambano ambalo litakuwa lake la pili nchini Kenya baada ya kusajili ushindi mwezi januari dhidi ya Wanyonyi.