ONYO LATOLEWA KWA WAZAZI WA ENEO BUNGE LA MALINDI

Msaidizi wa naibu wa kamishna wa eneo la Malindi kaunti ya Kilifi, Angela Wanyama amewaonya wazazi wa Malindi dhidi ya kuwaruhusu watoto wao kuhudhuria hafla za Disco matanga nyakati za usiku.
Kulingana na Wanyama kuwepo kwa Disco matanga katika jamii kumeathiri zaidi matokeo ya wanafunzi, wanaosoma katika taasisi mbalimbali za elimu mjini Malindi na kaunti ya Kilifi kwa jumla.
Akizungumza na wazazi pamoja na walimu katika mjini wa Malindi amesema idadi ya wanafunzi waliokuwa wanajiunga na shule za upili iliongezeka kwa kiasi kukubwa katika siku za nyuma, wakati ambapo idara ya usalama ilikuwa imepiga marufuku haflaza Dicso Matanga katika jamii.
Kwa upande wake mbunge wa Malindi kaunti ya Kilifi, Amina Mnyazi amesema ipo haja ya kuwepo kwa kikao kati ya viongozi wa idara ya usalama, walimu na baadhi ya wazazi ili kuzungumza kuhusiana na mikakati inayopaswa kutiliwa maanani ili kuboresha matokeo ya wanafunzi wa eneo bunge hili la Malindi.