Mchungaji wa kanisa la Ocean Assemblies Of God mjini Malindi kaunti ya Kilifi, Samuel Matiko amewaonya vijana dhidi ya kutizama filamu zilizo na video za ngono.
Kulingana na mchungaji huyo hatua ya vijana kutizama filamu hizo kumechangia pakubwa kwa ao, kuwa na hamu ya kushiriki ngono kabla ya ndoa.
Akizungumza na mwanahabari wetu katika afisini mwake, Matiko amewashauri vijana kuishi maisha ya matakatifu na kuhakikisha wanajitenga masuala hayo ya ngono kwani ni kinyume cha neno la Mungu.
Wakati uohuo ametoa wito kwa wachungaji na viongozi mbalimbali wa dini ya kikristo, kuzungumzia athari za vijana kujihusisha na ngono katika makongamano yanayowaleta vijana pamoja, ili waishi katika njia zinazompendeza Mwenyezi Mungu.
MCHUNGAJI MATIKO AWAONYA VIJANA DHIDI YA KUTAZAMA FILAMU ZILIZO NA VIDEO ZA NGONO

