Kocha wa timu ya Young Bulls Ali Said almaarufu Gaucho amesema anafurahia matokeo ya jana baadaya ya kuitandika timu ya Equity magoli 2-0 kwenye uga wa shule ya upili ya Malindi katika mashondano ya ligi ya daraja la kwanza humu nchini.
Gaucho amesema kwa sasa wako katika nafasi bora zaidi kujiunga na ligi kuu ya kitaifa “NSL” kufuatia ushindi huo ambao unamuacha mshindani wao wa karibu Nairobi United alama tano nyuma ya viongozi hao wa ligi ya daraja la kwanza nchini.
Hata hivyo Gaucho ameeleza ushirikiano wa timu pamoja na wachezaji wazoefu kwenye kikosi chake kama kiini cha mafanikio ya timu yake.
Kwa sasa Young Bulls wanaongoza jedwali la ligi hiyo wakiwa na alama 27 baada ya kucheza mechi 11 huku wakifuatwa na Nairobi United wenye alama 22 baada ya kucheza mechi 8.

