Klabu ya Gusii United imepewa alama tatu na shirikisho la fkf baada ya maamuzi ya kukatishwa kwa mechi yao dhidi ya Kajiado fc ugenini.
Baada ya tathmini ya kina na shirikisho kufuatia ripoti ya maafisa wa mechi hiyo ni kwamba Kajiado fc walifeli kuwasilisha gari la ambulensi uwanjani kwa mujibu wa sheria za maandalizi ya mechi.
Katika taarifa ya fkf iliyochapishwa mitandaoni ni kwamba klabu ya Gusii imepewa alama hizo tatu pamoja na mabao 2-0 katika mechi hiyo iliyoleta utata katika National Super League.

