MCHEZAJI WA KANTONGA FC YWAOMBA MSAADA WA MATIBABU

John King’oo nahodha wa klabu ya Kantonga kutoka kaunti ya Taita Taveta atakosekana kiwanjani kwa kipindi kirefu kutokana na kuvunjika mguu katika mechi ya Jumamosi ambapo Kantonga ilipigwa sare tasa dhidi ya klabu Yanga uwanjani Alaskan.

King’oo alivunjika mguu baada ya kugongana ana kwa ana Michael Agolla kipa wa Yanga.

Katika taarifa iliyochapishwa mitandaoni mchezaji huyo anaomba wahisani pamoja na wachezaji wenza katika ligi ya daraja la pili kusimama naye kimatibabu katika kipindi hiki kigumu kiuchumi.