Spika wa bunge la kaunti ya Lamu Azhar Mbarak ameitaka serikali kuu kufanyia marekebisho vitengo vya usalama ambavyo viko kwenye kaunti hiyo kama kubadilisha maafisa wa kitengo cha upelelezi NIS.
Mbarak amesema maafisa hao wanapaswa kuhamishwa na kupelekwa kwenye kaunti zingine na kisha kuletwa wengine wapya hatua ambayo amesema itamwezesha rais William Samoei Ruto kupata habari za uhakika kuhusiana na kaunti hiyo.
Kwa mujibu wa Mbarak maafisa wengine wamehudumu kwa miaka mingi na kuna haja ya wao kupewa uhamisho na kupongeza kuendelea kufanyiwa mageuzi kwa maafisa wakuu wa serikali kaunti ya Lamu akiwemo kamishna wa kaunti hiyo pamoja na kamanda wa polisi Lamu ambao wamepewa uhamisho.
AZHAR MBARAK AITAKA SERIKALI KUU KUFANYIA MAREKEBISHO VITENGO VYA USALAMA KAUNTI YA LAMU

